Jamaa anyongwa na nyama hadi kufa akisherehea mwaka mpya Kisii

August 2024 · 2 minute read

Jamaa mmoja kutoka kaunti ya Kisii amefariki dunia baada ya kunyongwa na nyama mbichi siku ya kusherehekea kufunga mwaka wa 2018

Osoro Oirere kutoka kijiji cha Sameta anasemekana alikuwa anahisi njaa sana na alijipata akiuuma kipande kikubwa cha nyama ambacho kilikwama kooni.

Habari Nyingine: Ruto amsaidia mbunge wa Ikolomani aliyejeruhiwa kufunga kamba za viatu vyake

Kulingana na taarifa tuliyoipokea hapa TUKO.co.ke, Osoro alikuwa nyumbani kwake wakati kisanga hicho kilipomtendekea.

Chifu wa eneo hilo Linus Choka alisema marehemu alikimbia nyumbani kwa kakake baada ya kugundua kwamba kipande kikubwa cha nyama kilikuwa kimekwama kwenye koo.

Inasemekana mkewe hakuwa nyumbani wala mtu yeyote ambaye angeweza kumsaidia.

Habari Nyingine: Jamaa aliyeachia shule darasa la 8 aunda gari jipya la KSh 300,000

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Kakake alisema alijaribu kumfanyia huduma ya kwanza ila juhudi zake hazikufaulu.

" Osoro alikuja nyumbani kwangu akikimbia huku akionyesha kidole chake kwenye koo , tulijaribu kumfanyia huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka katika zahanati ya Gentonto ila alifariki muda mfupi kabla ya kuhudumiwa na madaktari," Kakake marehemu alisema.

Habari Nyingine: Orodha ya watu 10 mashuhuri waliofariki 2018

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika kituo cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Lenmek ambapo jamii na marafiki walikusanyika na kuanza kufanya mipango ya mazishi.

Read: ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiboJzfZJmoZqlkZZ6orrYqKWgr5Fiu6J5zbKYppldna6ltYykrJ%2BZXZa4qr%2FHnqmeoJWWeq7DwKSYZqWgrq5ut8isoKJmmKm6rQ%3D%3D