Hesabu ya macho: Rais Uhuru hawezi kumuachia Raila kiti, Moses Kuria asema

September 2024 ยท 2 minute read

- Kuria alisema Raila anafaa kustaafu kwa sababu wakati wake wa kuongoza umepita

- Alisema historia ya Kenya inaonyesha rais humwachia kiti mgombea ambaye ni mchanga kumliko

- Kwa sasa Raila ni mzee kumshinda Uhuru na hivyo Kuria anasema kiti hicho kitaenda vingine

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amewataka wafuasi wa kinara wa ODM Raila Odinga wajue Rais Uhuru Kenyatta hawezi kumwachia kiti cha urais.

Kuria alisema Raila ni mzee kumliko Rais Uhuru n ahistoria imeonyesha ni watu wa umri wa chini kuliko rais aliye uongozini ambao humrithi.

Mbunge huyo aliwasimulia kuhusu safari ya siasa za urais tangu wakati wa Mzee Jomo Kenyatta had wakati wa Uhuru kuchukua usukani.

"Jomo alikuwa mzee kushinda Moi, akwamwachia, Moi alikuwa mzee kuliko Kibaki akamwachia, Kibaki alikuwa mzee kuliko Uhuru akwamwachia. Jamani, Uhuru anaweza wachia mzee kumshinda kweli? hii ni hesabu ya class two," Kuria alisema.

Habari Nyingine: DP Ruto atifua kivumbi kaunti ya Meru, apinga BBI

Kuria ni mmoja wa wafuasi sugu wa Naibu Rais William Ruto ambaye ametangaza wazi nia yake ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Ruto amekuwa akijipigia debe chini ya vuguvugu la Hustler Nation ambapo amewarai walala hoi kuunga safari yake ya Ikulu.

Habari Nyingine: Rais Uhuru amtupia vijembe DP Ruto kwa kushiriki kampeni za mapema za 2022

Kinara wa ODM Raila Odinga pia ameonyesha nia yake ya kutaka kuingia ikulu ifikapo 2022.

Kuria alisema Raila anafaa kustaafu kwa sababu wakati wake wa kuongoza ulipita ili awache nafasi hiyo kwa chipukizi wengine.

"Mimi namwambia rafiki yangu Raila Odinga astaafu polepole kwa sababu msimu ya kuwa rais imepita. Eti sasa ndio mtu akubali kushindwa baada ya uchaguzi ni lazima tubadilishe katiba. Kwa nini tubadilishe katiba kwa sababu mtu mmoja amekataa kukubadili kushindwa?" alisema Kuria.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbYJ4hZBmn56rkZfCbsXAZqSam5ikerOtyKxkrqClp8JutMCwnLOhXaDCrsHAnJ%2BimV2nrqq4wGaioqyZYrqwv8SsZKStop6ubq3SnqSaZpipuq0%3D